Surah Al-Layl (undefined) is the 92th chapter of the Holy Quran. It was revealed in Mecca and contains 21 verses (ayahs). Read it below with the Arabic text, transliteration, and Swahili translation, or open it as interactive flashcards to memorize it verse by verse.
- 92:1
وَٱلَّيْلِ إِذَا يَغْشَىٰ
Wallaili izaa yaghshaa
Naapa kwa usiku unapo funika!
- 92:2
وَٱلنَّهَارِ إِذَا تَجَلَّىٰ
Wannahaari izaa tajalla
Na mchana unapo dhihiri!
- 92:3
وَمَا خَلَقَ ٱلذَّكَرَ وَٱلْأُنثَىٰٓ
Wa maa khalaqaz zakara wal unthaa
Na kwa Aliye umba dume na jike!
- 92:4
إِنَّ سَعْيَكُمْ لَشَتَّىٰ
Inna sa'yakum lashattaa
Hakika juhudi zenu bila ya shaka ni mbali mbali.
- 92:5
فَأَمَّا مَنْ أَعْطَىٰ وَٱتَّقَىٰ
Fa ammaa man a'taa wattaqaa
Ama mwenye kutoa na akamchamngu,
- 92:6
وَصَدَّقَ بِٱلْحُسْنَىٰ
Wa saddaqa bil husnaa
Na akaliwafiki lilio jema,
- 92:7
فَسَنُيَسِّرُهُۥ لِلْيُسْرَىٰ
Fasanu yassiruhoo lilyusraa
Tutamsahilishia yawe mepesi.
- 92:8
وَأَمَّا مَنۢ بَخِلَ وَٱسْتَغْنَىٰ
Wa ammaa mam bakhila wastaghnaa
Na ama mwenye kufanya ubakhili, na asiwe na haja ya wenzake,
- 92:9
وَكَذَّبَ بِٱلْحُسْنَىٰ
Wa kazzaba bil husnaa
Na akakanusha lilio jema,
- 92:10
فَسَنُيَسِّرُهُۥ لِلْعُسْرَىٰ
Fasanu yassiruhoo lil'usraa
Tutamsahilishia yawe mazito!
- 92:11
وَمَا يُغْنِى عَنْهُ مَالُهُۥٓ إِذَا تَرَدَّىٰٓ
Wa maa yughnee 'anhu maaluhooo izaa taraddaa
Na mali yake yatamfaa nini atapo kuwa anadidimia?
- 92:12
إِنَّ عَلَيْنَا لَلْهُدَىٰ
Inna 'alainaa lal hudaa
Hakika ni juu yetu kuonyesha uwongofu.
- 92:13
وَإِنَّ لَنَا لَلْءَاخِرَةَ وَٱلْأُولَىٰ
Wa inna lanaa lal Aakhirata wal oolaa
Na hakika ni yetu Sisi Akhera na dunia.
- 92:14
فَأَنذَرْتُكُمْ نَارًۭا تَلَظَّىٰ
Fa anzartukum naaran talazzaa
Basi nakuonyeni na Moto unao waka!
- 92:15
لَا يَصْلَىٰهَآ إِلَّا ٱلْأَشْقَى
Laa yaslaahaaa illal ashqaa
Hatauingia ila mwovu kabisa!
- 92:16
ٱلَّذِى كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ
Allazee kazzaba wa tawallaa
Anaye kadhibisha na kupa mgongo.
- 92:17
وَسَيُجَنَّبُهَا ٱلْأَتْقَى
Wa sa yujannnabuhal atqaa
Na mchamngu ataepushwa nao,
- 92:18
ٱلَّذِى يُؤْتِى مَالَهُۥ يَتَزَكَّىٰ
Allazee yu'tee maalahoo yatazakkaa
Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa.
- 92:19
وَمَا لِأَحَدٍ عِندَهُۥ مِن نِّعْمَةٍۢ تُجْزَىٰٓ
Wa maa li ahadin 'indahoo min ni'matin tujzaaa
Na wala si kwa kuwa yupo yeyote aliye mfanyia hisani ndio anamlipa.
- 92:20
إِلَّا ٱبْتِغَآءَ وَجْهِ رَبِّهِ ٱلْأَعْلَىٰ
Illab tighaaa'a wajhi rabbihil a 'laa
Ila ni kutaka radhi ya Mola wake Mlezi aliye juu kabisa.
- 92:21
وَلَسَوْفَ يَرْضَىٰ
Wa lasawfa yardaa
Naye atakuja ridhika!
About Surah Al-Layl
Al-Layl, the Night, contrasts two kinds of people: the one who gives, is mindful of Allah, and believes in goodness, and the one who is stingy and turns away. It promises ease to the first and hardship to the second, teaching that our choices shape the path that opens before us.
Themes: Two paths, Generosity versus greed, Ease and hardship, Mindfulness of Allah
Arabic: Uthmani script (Hafs). Translation: Swahili. Recitation: Mishary Rashid Alafasy. See Sources for full attribution.