Surah Al-Inshiqaq (undefined) is the 84th chapter of the Holy Quran. It was revealed in Mecca and contains 25 verses (ayahs). Read it below with the Arabic text, transliteration, and Swahili translation, or open it as interactive flashcards to memorize it verse by verse.
- 84:1
إِذَا ٱلسَّمَآءُ ٱنشَقَّتْ
Izas samaaa'un shaqqat
Itapo chanika mbingu,
- 84:2
وَأَذِنَتْ لِرَبِّهَا وَحُقَّتْ
Wa azinat li Rabbihaa wa huqqat
Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza,
- 84:3
وَإِذَا ٱلْأَرْضُ مُدَّتْ
Wa izal ardu muddat
Na ardhi itakapo tanuliwa,
- 84:4
وَأَلْقَتْ مَا فِيهَا وَتَخَلَّتْ
Wa alqat maa feehaa wa takhallat
Na kuvitoa vilivyo kuwa ndani yake, ikawa tupu,
- 84:5
وَأَذِنَتْ لِرَبِّهَا وَحُقَّتْ
Wa azinat li Rabbihaa wa huqqat
Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza,
- 84:6
يَٰٓأَيُّهَا ٱلْإِنسَٰنُ إِنَّكَ كَادِحٌ إِلَىٰ رَبِّكَ كَدْحًۭا فَمُلَٰقِيهِ
Yaaa ayyuhal insaanu innaka kaadihun ilaa Rabbika kad han famulaaqeeh
Ewe mtu! Hakika wewe unajikusuru kwa juhudi kumwendea Mola wako Mlezi, basi utamkuta.
- 84:7
فَأَمَّا مَنْ أُوتِىَ كِتَٰبَهُۥ بِيَمِينِهِۦ
Fa ammaa man ootiya kitaabahoo biyameenih
Ama atakaye pewa daftari lake kwa mkono wa kulia,
- 84:8
فَسَوْفَ يُحَاسَبُ حِسَابًۭا يَسِيرًۭا
Fasawfa yuhaasabu hi saabai yaseeraa
Basi huyo atahisabiwa hisabu nyepesi,
- 84:9
وَيَنقَلِبُ إِلَىٰٓ أَهْلِهِۦ مَسْرُورًۭا
Wa yanqalibu ilaaa ahlihee masrooraa
Na arudi kwa ahali zake na furaha.
- 84:10
وَأَمَّا مَنْ أُوتِىَ كِتَٰبَهُۥ وَرَآءَ ظَهْرِهِۦ
Wa ammaa man ootiya kitaabahoo waraaa'a zahrih
Na ama atakaye pewa daftari lake kwa nyuma ya mgongo wake,
- 84:11
فَسَوْفَ يَدْعُوا۟ ثُبُورًۭا
Fasawfa yad'oo subooraa
Basi huyo ataomba kuteketea.
- 84:12
وَيَصْلَىٰ سَعِيرًا
Wa yaslaa sa'eeraa
Na ataingia Motoni.
- 84:13
إِنَّهُۥ كَانَ فِىٓ أَهْلِهِۦ مَسْرُورًا
Innahoo kaana feee ahlihee masrooraa
Hakika alikuwa furahani kati ya jamaa zake.
- 84:14
إِنَّهُۥ ظَنَّ أَن لَّن يَحُورَ
Innahoo zanna al lai yahoor
Huyo hakika alidhani kuwa hatarejea tena.
- 84:15
بَلَىٰٓ إِنَّ رَبَّهُۥ كَانَ بِهِۦ بَصِيرًۭا
Balaaa inna Rabbahoo kaana bihee baseeraa
Kwani? Hakika Mola wake Mlezi alikuwa akimwona!
- 84:16
فَلَآ أُقْسِمُ بِٱلشَّفَقِ
Falaaa uqsimu bishshafaq
Basi ninaapa kwa wekundu wa jua linapo kuchwa,
- 84:17
وَٱلَّيْلِ وَمَا وَسَقَ
Wallaili wa maa wasaq
Na kwa usiku na unavyo vikusanya,
- 84:18
وَٱلْقَمَرِ إِذَا ٱتَّسَقَ
Walqamari izat tasaq
Na kwa mwezi unapo pevuka,
- 84:19
لَتَرْكَبُنَّ طَبَقًا عَن طَبَقٍۢ
Latarkabunna tabaqan 'an tabaq
Lazima mtapanda t'abaka kwa t'abaka!
- 84:20
فَمَا لَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ
Famaa lahum laa yu'minoon
Basi wana nini hawaamini?
- 84:21
وَإِذَا قُرِئَ عَلَيْهِمُ ٱلْقُرْءَانُ لَا يَسْجُدُونَ ۩
Wa izaa quri'a 'alaihimul Quraanu laa yasjudoon
Na wanapo somewa Qur'ani hawasujudu?
- 84:22
بَلِ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ يُكَذِّبُونَ
Balil lazeena kafaroo yukazziboon
Bali walio kufuru wanakanusha tu.
- 84:23
وَٱللَّهُ أَعْلَمُ بِمَا يُوعُونَ
Wallaahu a'lamu bimaa yoo'oon
Na Mwenyezi Mungu anajua wanayo yadhamiria.
- 84:24
فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ
Fabashshirhum bi'azaabin aleem
Basi wabashirie adhabu chungu!
- 84:25
إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّٰلِحَٰتِ لَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍۭ
Illal lazeena aamanoo wa 'amilus saalihaati lahum ajrun ghairu mamnoon
Isipo kuwa wale walio amini na wakatenda mema; hao watakuwa na ujira usio malizika.
About Surah Al-Inshiqaq
Al-Inshiqaq, the Sundering, describes the sky being torn apart and the earth flattened on the Last Day, when every person meets the result of their striving. The one given his record in his right hand will return to his people in joy, while the one given it behind his back will call out in regret.
Themes: The Last Day, Meeting your deeds, The record of deeds, Striving
Arabic: Uthmani script (Hafs). Translation: Swahili. Recitation: Mishary Rashid Alafasy. See Sources for full attribution.