All Surahs

Surah Al-Qiyamah (undefined)

سُورَةُ القِيَامَةِ

Surah 75 of the Holy Quran · Meccan · 40 verses

Also spelled: Qiyamah, Al Qiyamah, AlQiyamah, The Resurrection

Surah Al-Qiyamah (undefined) is the 75th chapter of the Holy Quran. It was revealed in Mecca and contains 40 verses (ayahs). Read it below with the Arabic text, transliteration, and Swahili translation, or open it as interactive flashcards to memorize it verse by verse.

  1. 75:1

    لَآ أُقْسِمُ بِيَوْمِ ٱلْقِيَٰمَةِ

    Laaa uqsimu bi yawmil qiyaamah

    Ninaapa kwa Siku ya Kiyama!

  2. 75:2

    وَلَآ أُقْسِمُ بِٱلنَّفْسِ ٱللَّوَّامَةِ

    Wa laaa uqsimu bin nafsil lawwaamah

    Na ninaapa kwa nafsi inayo jilaumu!

  3. 75:3

    أَيَحْسَبُ ٱلْإِنسَٰنُ أَلَّن نَّجْمَعَ عِظَامَهُۥ

    Ayahsabul insaanu al lan najm'a 'izaamah

    Anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake?

  4. 75:4

    بَلَىٰ قَٰدِرِينَ عَلَىٰٓ أَن نُّسَوِّىَ بَنَانَهُۥ

    Balaa qaadireena 'alaaa an nusawwiya banaanah

    Kwani! Sisi tunaweza hata kuziweka sawa sawa ncha za vidole vyake!

  5. 75:5

    بَلْ يُرِيدُ ٱلْإِنسَٰنُ لِيَفْجُرَ أَمَامَهُۥ

    Bal yureedul insaanu liyafjura amaamah

    Lakini mtu anataka tu kuendelea na maasi kwa siku zilioko mbele yake.

  6. 75:6

    يَسْـَٔلُ أَيَّانَ يَوْمُ ٱلْقِيَٰمَةِ

    Yas'alu ayyyaana yawmul qiyaamah

    Anauliza: Lini itakuwa hiyo Siku ya Kiyama?

  7. 75:7

    فَإِذَا بَرِقَ ٱلْبَصَرُ

    Fa izaa bariqal basar

    Basi jicho litapo dawaa,

  8. 75:8

    وَخَسَفَ ٱلْقَمَرُ

    We khasafal qamar

    Na mwezi utapo patwa,

  9. 75:9

    وَجُمِعَ ٱلشَّمْسُ وَٱلْقَمَرُ

    Wa jumi'ash shamusu wal qamar

    Na likakusanywa jua na mwezi,

  10. 75:10

    يَقُولُ ٱلْإِنسَٰنُ يَوْمَئِذٍ أَيْنَ ٱلْمَفَرُّ

    Yaqoolul insaanu yaw ma 'izin aynal mafarr

    Siku hiyo mtu atasema: Yako wapi makimbilio?

  11. 75:11

    كَلَّا لَا وَزَرَ

    Kallaa laa wazar

    La! Hapana pa kukimbilia!

  12. 75:12

    إِلَىٰ رَبِّكَ يَوْمَئِذٍ ٱلْمُسْتَقَرُّ

    Ilaa rabbika yawma 'izinil mustaqarr

    Siku hiyo pa kutua ni kwa Mola wako Mlezi tu.

  13. 75:13

    يُنَبَّؤُا۟ ٱلْإِنسَٰنُ يَوْمَئِذٍۭ بِمَا قَدَّمَ وَأَخَّرَ

    Yunabba 'ul insaanu yawma 'izim bimaa qaddama wa akhkhar

    Siku hiyo ataambiwa aliyo yatanguliza na aliyo yaakhirisha.

  14. 75:14

    بَلِ ٱلْإِنسَٰنُ عَلَىٰ نَفْسِهِۦ بَصِيرَةٌۭ

    Balil insaanu 'alaa nafsihee baseerah

    Bali mtu ni hoja juu ya nafsi yake.

  15. 75:15

    وَلَوْ أَلْقَىٰ مَعَاذِيرَهُۥ

    Wa law alqaa ma'aazeerah

    Na ingawa atatoa chungu ya udhuru.

  16. 75:16

    لَا تُحَرِّكْ بِهِۦ لِسَانَكَ لِتَعْجَلَ بِهِۦٓ

    Laa tuharrik bihee lisaa naka lita'jala bih

    Usiutikisie huu wahyi ulimi wako kwa kuufanyia haraka.

  17. 75:17

    إِنَّ عَلَيْنَا جَمْعَهُۥ وَقُرْءَانَهُۥ

    Inna 'alainaa jam'ahoo wa qur aanah

    Hakika ni juu yetu kuukusanya na kuusomesha.

  18. 75:18

    فَإِذَا قَرَأْنَٰهُ فَٱتَّبِعْ قُرْءَانَهُۥ

    Fa izaa qaraanaahu fattabi' qur aanah

    Tunapo usoma, basi nawe fuatiliza kusoma kwake.

  19. 75:19

    ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا بَيَانَهُۥ

    Summa inna 'alainaa bayaanah

    Kisha ni juu yetu kuubainisha.

  20. 75:20

    كَلَّا بَلْ تُحِبُّونَ ٱلْعَاجِلَةَ

    Kallaa bal tuhibboonal 'aajilah

    Hasha! Bali nyinyi mnapenda maisha ya duniani,

  21. 75:21

    وَتَذَرُونَ ٱلْءَاخِرَةَ

    Wa tazaroonal Aakhirah

    Na mnaacha maisha ya Akhera.

  22. 75:22

    وُجُوهٌۭ يَوْمَئِذٍۢ نَّاضِرَةٌ

    Wujoohuny yawma 'izin naadirah

    Zipo nyuso siku hiyo zitao ng'ara,

  23. 75:23

    إِلَىٰ رَبِّهَا نَاظِرَةٌۭ

    Ilaa rabbihaa naazirah

    Zinamwangallia Mola wao Mlezi.

  24. 75:24

    وَوُجُوهٌۭ يَوْمَئِذٍۭ بَاسِرَةٌۭ

    Wa wujoohuny yawma 'izim baasirah

    Na zipo nyuso siku hiyo zitakao kunjana.

  25. 75:25

    تَظُنُّ أَن يُفْعَلَ بِهَا فَاقِرَةٌۭ

    Tazunnu any yuf'ala bihaa faaqirah

    Zitajua ya kuwa zitafikiwa na livunjalo uti wa mgongo.

  26. 75:26

    كَلَّآ إِذَا بَلَغَتِ ٱلتَّرَاقِىَ

    Kallaaa izaa balaghatit taraaqee

    La, hasha! (Roho) itakapo fikia kwenye mafupa ya koo,

  27. 75:27

    وَقِيلَ مَنْ ۜ رَاقٍۢ

    Wa qeela man raaq

    Na pakasemwa: Nani wa kumganga?

  28. 75:28

    وَظَنَّ أَنَّهُ ٱلْفِرَاقُ

    Wa zanna annahul firaaq

    Na mwenyewe akajua kwa hakika kuwa huko ndiko kufariki;

  29. 75:29

    وَٱلْتَفَّتِ ٱلسَّاقُ بِٱلسَّاقِ

    Waltaffatis saaqu bissaaq

    Na utapo ambatishwa muundi kwa muundi,

  30. 75:30

    إِلَىٰ رَبِّكَ يَوْمَئِذٍ ٱلْمَسَاقُ

    Ilaa rabbika yawma'izinil masaaq

    Siku hiyo ndiyo kuchungwa kupelekwa kwa Mola wako Mlezi!

  31. 75:31

    فَلَا صَدَّقَ وَلَا صَلَّىٰ

    Falaa saddaqa wa laa sallaa

    Kwa sababu hakusadiki, wala hakusali.

  32. 75:32

    وَلَٰكِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ

    Wa laakin kazzaba wa tawalla

    Bali alikanusha, na akageuka.

  33. 75:33

    ثُمَّ ذَهَبَ إِلَىٰٓ أَهْلِهِۦ يَتَمَطَّىٰٓ

    Summa zahaba ilaaa ahlihee yatamatta

    Kisha akenda kwa ahali zake kwa matao.

  34. 75:34

    أَوْلَىٰ لَكَ فَأَوْلَىٰ

    Awlaa laka fa awlaa

    Ole wako, ole wako!

  35. 75:35

    ثُمَّ أَوْلَىٰ لَكَ فَأَوْلَىٰٓ

    Summa awlaa laka fa awla

    Kisha Ole wako, ole wako!

  36. 75:36

    أَيَحْسَبُ ٱلْإِنسَٰنُ أَن يُتْرَكَ سُدًى

    Ayahsabul insaanu anyytraka sudaa

    Ati anadhani binaadamu kuwa ataachwa bure?

  37. 75:37

    أَلَمْ يَكُ نُطْفَةًۭ مِّن مَّنِىٍّۢ يُمْنَىٰ

    Alam yaku nutfatam mim maniyyiny yumnaa

    Kwani hakuwa yeye tone ya manii lilio shushwa?

  38. 75:38

    ثُمَّ كَانَ عَلَقَةًۭ فَخَلَقَ فَسَوَّىٰ

    Summa kaana 'alaqata fakhalaq fasawwaa

    Kisha akawa kidonge cha damu, tena Mwenyezi Mungu akamuumba na akamtengeneza vilivyo.

  39. 75:39

    فَجَعَلَ مِنْهُ ٱلزَّوْجَيْنِ ٱلذَّكَرَ وَٱلْأُنثَىٰٓ

    Faja'ala minhuz zawjayniz zakara wal unsaa

    Kisha akamfanya namna mbili, mwanamume na mwanamke.

  40. 75:40

    أَلَيْسَ ذَٰلِكَ بِقَٰدِرٍ عَلَىٰٓ أَن يُحْۦِىَ ٱلْمَوْتَىٰ

    Alaisa zaalika biqaadirin 'alaaa any yuhyiyal mawtaa

    Je! Huyo hakuwa ni Muweza wa kufufua wafu?

About Surah Al-Qiyamah

Al-Qiyamah, the Resurrection, answers those who doubted that Allah could bring the dead back to life. It points out that Allah can reassemble even the tips of a person's fingers, describes the moment the eyes are dazzled and the soul reaches the throat, and reminds the human being that they were created for a purpose, not left without account.

Themes: The resurrection, Power of the Creator, The moment of death, Purpose

Arabic: Uthmani script (Hafs). Translation: Swahili. Recitation: Mishary Rashid Alafasy. See Sources for full attribution.